Jumla wa wagombea wanane wamepitishwa kuwania ubunge jimbo
la Monduli mkoa wa Arusha
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, leo Agosti 21
Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo la Monduli, Stevin Ulaya amesema wagombea
wote wamepitishwa baada ya kukidhi matakwa ya uchaguzi
Ulaya amewataja wagombea hao kuwa ni Julius Kalanga (CCM),
Yonas Laizer(Chadema) na Omar Kawanga(DP).
Wengine ni Feruzi Juma (NRA), Simon Ngilisho (Demokrasia
Makini),Fransis Ringo(ADA-TADEA).</p></div><div><p>Ulaya
amewataja wagombe wengine waliopitishwa kuwa ni pamoja na Elizabeth Salewa
(AAFP) na Wilfred Mlay (ACT-Wazalendo).
Hata hivyo katika uchaguzi huo,Upinzani mkubwa upo kati ya
wagombea wa CCM na Chadema ambao wanatoka kata moja ya Lepurko
Laizer ambaye pia ni diwani wa kata alipitishwa kugombea kwa
tiketi ya Chadema na atachuana na Kalanga wa CCM katika uchaguzi wa Septemba 16
Mkazi wa Monduli, Lenana Mollel alizungumzia kinyang’anyiro
hicho na kusema hata kabla ya Kalanga kuhamia Chadema alikuwa akipambana na
Laizer hivyo wao kuwania jimbo hili kunaongeza makali
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Loota Sanare ametamba kuwa
tayari CCM imeshinda uchaguzi huo kwani inakubalika Monduli
"Monduli wamejua makosa waliyofanya sasa wameona kazi
nzuri za serikali na wanaiunga mkono," amesema
Mwenyekiti wa Chadema mkoa Arusha, Aman Golugwa ametaka
uchaguzi uwe huru na haki na kusema kuwa wanauhakika wa ushindi asubuhi
"Tumejipanga kutetea jimbo tunajua wana Monduli
wanahasira baada ya Kalanga kurubuniwa na kuwatoroka ila hasira zao zitaonekana
siku ya uchaguzi," amesema
Uchaguzi huo utafanyika Septemba 16 baada ya aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo, Kalanga, kutangaza kukihama Chadema na kuhamia CCM
Wagombea wanane wapitishwa Monduli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment