Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga amehudhuria
mazishi ya dada yake Rais John Magufuli aliyezikwa leo kijiji cha Mlimani,
Chato
Pamoja na Odinga, marais wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan
Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
pia walihudhuria mazishi ya dada huyo wa Rais, Monica Joseph Magufuli
Monica alifariki dunia Jumapili Agosti 19 katika Hospitali
ya Bugando alikokuwa akipata matibabu
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo Agosti 21, imemkariri
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Mawasiliano wa Ikulu Gerson Msigwa kuwa, Misa ya
mazishi ya imeongozwa na Askofu wa Jimbo la Katoliki la Rulenge Mhashamu
Severine Niwemuguzi aliyeambatana na maaskofu wengine saba
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni , Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi, Mawaziri, Wabunge, Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama,
Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wengine
mbalimbali wa Mikoa, Wilaya, Taasisi, Idara na Kampuni
Taarifa hiyo imesema marehemu Monica ameacha watoto tisa,
mume na wajukuu 25
Katika salamu zake Rais Magufuli amewashukuru viongozi na
wananchi wote waliojitokeza kuungana na familia katika kumsindikiza dada yake
katika safari yake ya mwisho
“Mmetuonesha upendo mkubwa sana na kweli ujio wenu na
kuungana nasi katika tukio hili mmetufariji sana, asante sana kwa upendo huu na
Mungu awabariki sana, ”amesema Magufuli
Rais Magufuli amemuelezea Dada yake Monica kuwa alikuwa mtu
mwenye upendo kwa familia nzima na alikuwa tegemeo kubwa la kumtunza mama yao
mzazi Suzana Ngolo Magufuli
“Alikubali kuondoka nyumbani kwa mumewe kwa zaidi ya miaka
miwili na kurudi nyumbani kumlea mama yetu mzazi,” amesema Rais Magufuli katika
taarifa yake
Odinga amfariji Magufuli msiba wa dada yake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment