Naibu Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde amewataka wananchi kujenga
utaratibu wa kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa ili kujikinga na
kujiandaa na maafa yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi
Ametoa rai
hiyo leo Jumanne Agosti 21, 2018 katika uzinduzi wa Mfumo wa Taifa wa Huduma za
Hali ya Hewa (NFCS) jijini hapa
Amesema ili
nchi iweze kupata maendeleo, utekelezaji wa udhibiti
wa majanga yatokanayo na
hali ya hewa ni muhimu kuzingatiwa
“Mfano
asilimia 60 ya wananchi wamejikita katika kilimo na uvuvi lakini hawawezi
kufanikiwa kama kazi zao zitaathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa,"
amesema Mavunde na kuwataka wananchi kutofuata utabiri wa hali ya hewa wa
mitaani
“Watu wanapuuza
utabiri wa hali ya hewa na kujikuta wakipata madhara makubwa ikiwemo
mafuriko na kusababisha wengine kukosa makazi ya kuishi.”
Amebainisha
kuwa magonjwa ya mimea, wakulima kukosa mavuno na kuongezeka kwa kina cha
bahari ni moja ya athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa,
kubainisha kuwa ni muhimu kuzingatia utabiri sahihi na wa kitaalam
Amesema mfumo
huo wa NFCS utasaidia kuboresha utoaji wa taarifa na matumizi ya huduma za hali
ya hewa na kufanya maamuzi mapema
"Pia
lengo ni kuwajengea uwezo wananchi kuhusu athari zitokanazo na mabadiliko ya
hali ya hewa kwa sababu wengi wamekuwa wagumu kufuatilia taarifa mbalimbali,”
amesema
Kwa upande
wake mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Agnes Kijazi
amesema licha ya wananchi kuwa na uelewa wa kufuatilia taarifa za hali ya hewa
bado uzingatiaji unahitajika ili kukabiliana zaidi na athari zinazotokea
Amebainisha
kuwa mfumo huo utasaidia kuboresha matumizi sahihi ya hali ya hewa na kupunguza
majanga ikiwemo mafuriko ambayo hutokea mara kwa mara
"Tanzania
kama nchi nyingine mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo ukame, mafuriko na
maradhi vinaweza kuepukika endapo tutaendelea kuwajengea uwezo watoaji na
watumiaji wa huduma za hali ya hewa," amesema.
Mavunde awataka wananchi kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment