WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameendelea
kuwabana polisi akiwataka kuachana na tabia ya kubambikia raia kesi zikiwamo za
uzururaji na ugaidi
Lugola alitoa kauli hiyo Jumatatu jioni baada ya kufanya
ziara ya kikazi katika Chuo cha Taaluma cha Polisi Kurasini jijini Dar es
Salaam na kuzungumza na maofisa wa chuo hicho na wanafunzi
Alisema aliamua kufanya ziara hiyo baada ya kupokea
malalamiko mengi kutoka kwa raia kuhusu kubambikwa kesi na askari polisi
"Miongoni mwa kesi ambazo raia wanalalamikia
kubambikiwa sana ni uzururaji na kesi za ugaidi," Lugola alisema
Waziri huyo aliongeza kuwa, kuna maofisa wenye vyeo ndani ya
jeshi hilo aliokutana nao lakini kutokana na vitendo vyao amewatilia shaka kama
kweli waliwahi kupitia mafunzo chuoni hapo
"Kuna baadhi ya mambo yanayofanyika kule chini ambayo
yananishangaza sana, nimekuwa nikijiuliza jeshi hili ni la weledi na wa kisasa
kweli? Yuko OCS mmoja (Mkuu wa Kituo) kama ninyi, yupo kwenye kituo cha polisi
"Yeye kila kukicha asilimia 90 ya watu ambao
anawakamata na kuwaweka ndani wote ni dili analotengeneza yeye, najiuliza ina
maana siku hizi tunakwenda kusoma tuje kutengeneza madili?"
Moyo wa kufukuzia madaraka haupo, nimeona umuhimu wa mafunzo
haya pengine mimi nikisema mtabadilika na ninyi wakati mnasoma mtakuja
kunikumbuka siku moja kuwa alikuja waziri akatukumbusha
"Si lazima uchafuke mabega upate madaraka, kuna watu
wamechafuka mabega lakini ndiyo hao wa madili... kuna watu hawajachafuka
wanafanya kazi vizuri, wapo huko vituoni."
Waziri huyo aliwataka maofisa na askari chuoni hapo
kuhakikisha wanatumia mafunzo hayo kulinda usalama wa raia na siyo
kuwakandamiza kwa kuwabambikia kesi mbalimbali.
Lugola azidi kuwabana Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment