Mabasi mawili ya wanafunzi Shule ya Kivulini na Shule ya
Nyamunge yamengana uso kwa uso katika Barabara ya Mwanza – Simiyu katika
eneo la Nane nane mkoani Mwanza na kusababisha kifo cha dereva na kujeruhiwa
wanafunzi wanane wa shule hizo
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahamed
Msangi, amesema aliyefariki katika ajili hiyo ni dereva wa basi la shule ya
Nyamuge Albert Joram (58
Kamanda Msangi ambaye amehamishiwa makao makuu ya Jeshi la
Polisi Dar es salaam, amesema katika ajali hiyo wanafunzi wanane na dereva wa
gari la shule ya Kivulini, Kulwa Mayala (27), wamepata majeraha
sehemu mbalimbali za miili yao hasa miguuni
“Majeruhi hao walikimbizwa katika kituo cha afya cha
Buzuruga na baadae mwanafunzi mmoja alilazimika kuhamishiwa hospitali ya
rufaa, Bugando kwa matibabu zaidi huku wawili wakilazwa katika hospitali ya
Sekou Toure jijini Mwanza,”amesema Kamanda Msangi.
Mabasi ya Shule yagongana uso kwa uso mmoja afariki
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment