Wananchi wa kata ngaranaro jijini arusha wameanza
kuondokana na Changamoto ya mafuriko iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu na
Kuwasababishia wananchi hao hasara ya mali pamoja na Nyumba zao kubebwa na
mafuriko kila Mvua inaponyesha.
Akizungumza Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqaro
alipotembelea katika kata hiyo amekagua jinsi mtaro unavyojengwa amesema mpaka
kukamilika kwake utagharimu Sh Milioni 295 .
Daqaro Amesema kuwa kipindi cha Mvua kulikuwa na
changamoto kubwa za wananchi kuingiliwa na maji katika makazi yao hivyo kupitia
ujenzi huo utarahisisha kutatua tatizo hilo lililokuwepo kama hali ya hewa itaendelea kuwa
nzuri na mvua za kawaida.
Pamoja na hayo amewataka viongozi wa ngazi ya kata kuhakikisha wanasimamia kwa
umakini ujenzi huo pamoja na kusimamia wananchi wasitupe taka katika mtaro huo
unaojengwa kwa fedha nyingi.
Naye meneja wa mamlaka ya usimamizi wa barabara
Mkoa wa Arusha Eng John Kalupale amesema kuwa urefu wa mtaro huo ni Mita 313 na
utajengwa kwa miezi 2 lakini kutokana na kasi ya Mkandarasi pamoja na mafundi
wanaofanya kazi hiyo itafanyika kwa mwezi mmoja na nusu.
Eng
Kalupale amesema kuwa kila mwananchi anatakiwa kuwa kipao mbele kulinda
miundombinu inayoletwa na serikali ambayo inamanufaa kwa wananchi wote kwa
ujumla na kuunga mkono juhudi zilizopo kwa kuwa kuna baadhi wanaona kuwa ni
kama kero kwa kuwa inapita maeneo yao.
Wananchi
wa kata ya Ngarenaro wameishukuru serikali kwa kuwajengea mtaro huo kwasababu
kila kipindi cha mvua kinapofika wengi huteseka kutokana na mafuriko kuingia
katika makazi yao na wengine kuhama kipindi cha Mvua.
Serikali yawaondolea Wananchi Maafa yaliyokuwepo tangu Mkoloni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment