Rais John Magufuli amewashukuru watanzania na viongozi wa
serikali waliojitokeza kumfariji wakati wa msiba wa dada yake, Monica Joseph
Magufuli
Monica alifariki dunia Agosti 19 mwaka huu na kuzikwa Agosti
21 katika kijiji cha Mlimani, Chato, Geita
Rais Magufuli amesema upendo na ushirikiano uliooneshwa na
kila aliyeguswa na kifo cha dada yake umemfariji kwa kiasi kikubwa yeye na
familia nzima na umewatia nguvu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha
majonzi
“Kifo cha Dada yangu Monica, kimesababisha huzuni na majonzi
makubwa kwetu sisi wanafamilia kwa kuwa tulimtegemea kwa mengi na ndiye alikuwa
akimlea Mama yetu Suzana Ngolo Magufuli, lakini salamu za pole, maombi
yenu na tulipowaona wengi mmekuja kuungana nasi kumsindikiza katika safari ya
mwisho, tumefarijika sana na tumepata nguvu
“Kwa niaba ya familia naomba kuwashukuru sana nyote kwa moyo
wenu wa upendo na maombi yenu, naamini mtaendelea kuungana nasi kumuombea dada
yetu Monica apumzike mahali pema peponi, Amina” amesema Rais Magufuli
Rais Magufuli awashukuru watanzania
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment