Mgombea udiwani wa CCM Monduli apita bila kupingwa


Mgombea wa Udiwani wa CCM Kata ya Mswakini wilayani Monduli, Nanga Lenasira Mollel amepita bila kupingwa

Ofisa Uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Monduli, Meleji Kuresoi amesema hadi leo saa 10 jioni hakuna mgombea wa upinzani aliyejitokeza

"Tulitangaza muda wa kuchukua fomu na kurejesha lakini hadi leo jioni amechukua Lenasira pekee na kurejesha" amesema

Amesema kutokana na taratibu za uchaguzi zilivyo mgombea huyo amepita bila kipingwa

Awali Diwani huyo alikuwa ni wa Chadema na alijiuzulu na kujiunga na CCM na kuchukua fomu kutetea nafasi yake

Hadi sasa jumla ya madiwani 10 wa Chadema wilaya ya Monduli wamejiuzulu na kujiunga na CCM

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi Monduli, Stevin Ulaya sasa halmashauri ya Monduli ambayo awali ilikuwa ya Chadema kutokana na kuwa na madiwani 18 na CCM 9 tu imekuwa ya CCM

Kwa sasa CCM imekuwa na madiwani 17 huku Chadema ikibaki na tisa

Mgombea udiwani wa CCM Monduli apita bila kupingwa Mgombea udiwani wa CCM Monduli apita bila kupingwa Reviewed by KUSAGANEWS on August 23, 2018 Rating: 5

No comments: