Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, Constantine Mathias,
amehojiwa na polisi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao na kujihusisha na
vitendo vya rushwa
Akizungumza leo Agosti 23 Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu,
Deusdedit Nsimeki amesema Mathias alikamatwa, akahojiwa kisha akaachiwa
Imeelezwa kuwa Mathias alisambaza picha kwenye mtandao wa
kijamii wa facebook inayomuonyesha askari polisi akinywa bia akiwa na sare za
kazi
Picha anazodaiwa kusambaza ni za askari polisi PC Neto
Mahenge wa kituo cha polisi Mwamapalala
"Anahojiwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao ya
kijamii na madai ya kujihusisha na vitendo vya rushwa. Nimeagiza achukuliwe
maelezo na kuachiwa kwa dhamana akikamilisha taratibu na mahitaji ya
kisheria," amesema Kamanda Nsimeki
Mwandishi wa habari matatani kwa kusambaza picha za polisi akiwa baa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment