Shirika la viwango nchini TBS
limebaini kuwepo kwa nyaya na vifaa vingine vya kupitishia umeme vinavyouzwa
kwenye maduka kariakoo huku vifaa hivyo vikiwa havina ubora.
Mratibu wa
ukaguzi huo, Simon Emmanuel na Afisa Udhibiti Ubora, Daudi Nkugile wamesema
shirika hilo litalazimika kuteketeza vifaa hivyo kwa gharama za wenye mali ili
iwe fundisho kwa wafanyabiashara wenye tabia ya kuingiza sokoni bidhaa zisiso
na viwango au zenye viwango hafifu.
Wakizungumza wakati wa zoezi la ukaguzi wa bidhaa mbali mbali kwenye maduka yaliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam, maafisa wa TBS wamesema vifaa vilivyokamatwa ni hatari kwa usalama wa majengo na maisha ya watumiaji.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wakati akisoma bajeti ya wizara yake Bungeni mjini Dodoma, alisema kuwa watumishi wa umma watakaoruhusu bidhaa feki Julai mosi mwaka huu, kuingia kwenye soko la ndani wajiandae kuachia nafasi zao.

TBS yakamata vifaa feki vya umeme
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 24, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment