Mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Kagoma, Belina
Bonifasi (9) mkazi wa kijiji cha Kagoma wilayani hapa mkoani Kagera amefariki
dunia leo Ijumaa Agosti 24, 2018, ikielezwa kuwa amepigwa na radi
Akizungumza leo mzazi wa mwanafunzi huyo, Renatus
Pastory amesema mwanae alikutwa na umauti wakati akijiandaa kwenda shule baada
ya radi kupiga dirishani
“Ameungua upande wa kulia wa mwili wake. Alikuwa akiandaliwa
chai na mama yake ili aweze kwenda shule,” amesema
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Jeremiah Januari amesema
mwanafunzi huyo alikuwa miongoni mwa wanafunzi 115 wa darasa la pili
shuleni hapo na kubainisha kuwa wamepokea taarifa za kifo hicho kwa mshtuko
Chanzo:Mwananchi
Mwanafunzi afariki dunia, adaiwa kupigwa na radi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 24, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment