Jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu 13 kwa
tuhuma za mauaji ya wanawake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa
Akizungumza Kamanda wa operesheni wa polisi, Liberatus Sabas
amesema watuhumiwa hao wametiwa mbaroni wakihusishwa na mauaji ya wanawake 29
katika mikoa ya Geita, Mwanza na Shinyanga
"Hawa ni pamoja na kinara wao tuliyemtia mbaroni juzi
wilayani Misungwi," amesema Sabas
Amesema watuhumiwa hao wamenaswa katika operesheni maalum
inayoendeshwa na polisi tangu Agosti 2017 katika mikoa hiyo ambako kunatokea
mauaji yenye utata ya wanawake ambao licha ya kunyongwa, pia hukatwa
baadhi ya viungo vya mwili ikiwemo sehemu za siri
"Tangu mwaka jana tunafanya operesheni maalum ya kimya
kimya dhidi ya wanaowavamia, kuwaua na kuwakata baadhi ya viungo wanawake, hasa
katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Geita," amesema Sabas
Miongoni mwa walionaswa kwa mujibu wa mkuu huyo wa
operesheni wamo waganga wa jadi, watekelezaji wa mauaji, wanaopanga, kuratibu,
kisimamia na kufadhili mauaji hayo
13 wadakwa Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya wanawake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 24, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment