Rais Yoweri Museveni amesema kwamba, yeye kama mkuu wa nchi,
hana mamlaka ya kumwachia huru Mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi
pamoja na wenzake waliokamatwa na polisi
"Rais wa Uganda hana mamlaka kama hayo," amesema
katika taarifa yake iliyofuatia mkasa uliotokea wakati wa uchaguzi mdogo wa
Jimbo la manispaa ya Arua
"Mara mtu akikamatwa, akashtakiwa na kuwekwa mahabusu,
ni mamlaka mbili tu ambazo zinaweza kuwatoa watu hao kwa namna yoyote,"
anasema Rais Yoweri Museveni
Katika taarifa ndefu aliyoitoa Jumatano, Museveni pia
alilaani namna waandishi wa habari walivyopigwa na vyombo vya usalama
Katika taarifa iliyokuwa ujumbe kwa wananchi wa Uganda
Museveni alisema, “Nimesoma maoni yenu kuhusiana na kauli yangu ya awali.
Ninawashukuru nyote kwa kutoa maoni yenu. Hii ndiyo njia nzuri na yenye manufaa
kwa kuwasiliana; hakuna haja ya vurugu na "fujo".
Hata hivyo, kuna kitu kimoja ambacho watu hawataki
kukielezea katika maoni yao. Hicho ni suala la ukosefu wa ajira kwa vijana
mijini na vijijini.
Hicho ni moja ya vipengele, ukweli ni kipengele kikuu,
wanasiasa wasio na misingi (wanaojijali masilahi yao na wanaoweka kando
taratibu zinazokubalika kufikia mafanikio) wanakitumia kuwashawishi vijana wetu
kuingia kwenye na fujo,” alisema
Museveni: Sina uwezo kumtoa Bobi Wine
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 24, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment