Mahakama Kuu nchini Zimbabwe, imetupilia mbali kesi
iliyofunguliwa na chama cha upinzani nchini humo, MDC ya kupinga matokeo ya
uchaguzi yaliyompa ushindi, Emmerson Mnangagwa
“Katika uchunguzi wake Mahakama imebaini kuwa mlalamikaji
ameshindwa kuonyesha ushahidi kamili na wa moja kwa moja kwamba uchaguzi
uligubikwa na kasoro” amesema Jaji Mkuu Luke Malaba wakati akitangaza uamuzi huo
katika mahakama ya Katiba, jijini Harare
Oktoba mwaka jana, Mnangangwa alimrithi Robert Mugabe
aliyetawala Zimbabwe kwa zaidi ya miaka 37
Katika uchaguzi huo uliofanyika Agosti mwaka huu, Zanu-PF
kilishinda kwa asilimia 50.8 ya kura zote na chama cha upinzani cha MDC
kilipata asilimia 44.3 ya kura hizo
Katika kesi hiyo, majaji tisa wakiongozwa na Jaji Mkuu
Malaba, walitoa uamuzi huo huku ulinzi katika eneo la Mahakama ukiimarishwa
Kwa mara ya kwanza nchini humo, kesi hiyo ilirushwa moja kwa
moja na televisheni ya taifa
Mahakama yampa ushindi Mnangagwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 24, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment