Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa chama cha Mapinduzi
(UWT) Queen Mlozi ameitaka jamii kukemea kauli za kejeli zinazotolewa pindi
mwanamke anapoteuliwa katika nafasi ya uongozi
Mlozi ameyasema hayo leo Agosti 23 jijini Dar es Salaam
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyofikiwa katika
utekekezaji wa ilani ya CCM
Amesema anasikitishwa na kauli hizo kwa kuwa zinalenga
kuwakatisha tamaa wanawake na kuwafanya washindwe kujiamini.
Mlozi amesema kwa mwenendo huo upo uwezekano hata anayefanya
uteuzi akakata tamaa kwa kuwa akiteuliwa mwanamke kauli zisizofaa zinatolewa
"Wanawake tuwe mstari wa mbele kukemea kauli hizi
kwa kuwa si nzuri na zinalenga kuturudisha nyuma
"Kwanza tujiulize kwanini kejeli zinaibuka akiteuliwa
mwanamke, tuelimishane, tuzungumze na tukemee haya kwa umoja wetu,” amesema
“Ni lazima ifike mahali tuseme hapana itafika wakati hata
anayetuteua atapata ukakasi. Tusikatishane tamaa katika vitu vya
msingi."ameongeza
Mlozi ametumia fursa hiyo kumuomba Rais John Magufuli
kuendelea kuwaamini na kuwateua wanawake kwa kuwa wanaweza kufanya kazi
kwa uaminifu mkubwa
Katibu Mkuu UWT akemea wanaokejeli uteuzi wa wanawake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment