Chadema kanda ya kati kimesema kitawaumia wabunge wake
kulinda kura wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kizota jijini hapa
unaotarajiwa kufanyika Septemba 16, 2018
Hayo yamesemwa leo Agosti 23 na Katibu wa Chadema kanda ya
kati, Iddi Kizota muda mfupi baada ya mgombea wa chama hicho kurudisha fomu ya
kugombea udiwani
Amesema wamefikia uamuzi huo baada ya baadhi ya mawakala
wanaowekwa vituoni kujiondoa siku ya kupigra kura
"Ikiwezekana tutatumia hata wabunge na ukiangalia
uchanguzi unafanyika Septemba 16,2018 kipindi ambacho Bunge linaendelea na
vikao vyake basi wabunge 19 tutaweza kuwapata,"
"Katika kata yetu ya Kizota tuna vituo vya kupigia kura
19 hivyo hao wabunge 19 ni kwa ajili ya kuwa mawakala kwenye vituo vya kupigia
kura," amesema Kizota
Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata ya Kizota
kupitia Chadema Omary Bangababo amesema kuwa ameamua kuchukua fomu ya
kugombea nafasi hiyo ili kuwatumikia wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua kero
ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kizota ya kutokuwa na maabara
Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Kizota Loyce Mrefu
amesema hada sasa wawakilishi wote vyama sita waliochukua fomu kwa nafasi
hiyo ya udiwani wamekwisharejesha fomu zao
Waliorudisha fomu ni Jamali Ngalya (CCM), Salum Salum
(CUF), Omary Bangababo (Chadema), Jacklin Msajila (UPDP), Aziz Abas (NCCR-
Mageuzi) pamoja na Peter Malya (NLD).
Chadema kutumia wabunge wake kulinda kura uchaguzi mdogo Septemba 16
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment