Mkazi wa Vingunguti, Seleman Mohamed (18), amefikishwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu shtaka la kumpa mwanafunzi
mimba
Mohamed amepandishwa mahakamani hapo leo Agosti 23, mbele ya
Hakimu Mkazi Eliarusia Nassary na kusomewa shtaka moja la kumpa mimba
mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17.
Wakili wa Serikali, Ashura Mzava, amedai mshitakiwa alitenda
kosa hilo kati ya Aprili na Juni, 2018 eneo la Vingunguti wilayani Ilala
Mshtakiwa anadaiwa siku hiyo ya tukio huku akijua kufanya
hivyo ni kinyume cha sheria, alimpa mimba mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17.
Hata hivyo, mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka
linalomkabili, alikana shitaka hilo ambapo upande wa mashitaka ulidai upelelezi
wa shauri hilo bado haujakamilika na hivyo kuomba tarehe nyingine ya kutajwa
Hakimu Eliarusia ametaja masharti ya dhamana ambayo ni
wadhamini wawili mmoja kati yao awe mwajiriwa watakaosaini dhamana ya
Sh1milioni kila mmoja
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na
kurudishwa rumande hadi Septemba 4, mwaka huu, kesi yake itakapotajwa
Katika hatua nyingine, Athuman Mohamed (18), amefikishwa
mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la kukutwa na dawa za kulevya aina ya
bangi zenye uzito wa kilogramu 3.55
Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Flora
Mujaya, wakili wa Serikali Sylvia Mitanto, alidai mshtakiwa alikutwa na kiasi
hicho cha bangi Agosti 7, 2018, eneo la Kivule Matembele wilayani Ilala
Mshitakiwa alikana shitaka hilo na upande wa mashtaka
walidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na hivyo kuomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kutajwa
Hakimu Flora ametaja masharti ya dhamana kuwa, mshtakiwa
anatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja kati yao awe na barua kutoka
sekta yoyote inayotambulika watakaosaini dhamana Sh 1milioni moja kila
mdhamini
Apandishwa kizimbani kwa kumpa mimba mwanafunzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment