Mashirikia yasiyokuwa ya Kiserikali (NGO’s) yametakiwa kutokuwa
chanzo cha Migogoro ya Kisiasa kwa wananchi bali yasimamie Sheria na Taratibu
zinazowaongoza kwa kufuata makubaliano yaliyofanya na serikali pamoja na kutambuliwa
rasmi kwa ajili ya kushirikiana na wananchi
Wilaya ya Longido ina mashirika yasiyo ya kiserikali
zaidi ya 30 ambayo yote yamesajiliwa na serikali kwa ajili ya kushirikiana na
wananchi.
Hayo yametanabaishwa na Mkuu wa wilaya ya Longido Mkoani
Arusha Bwana Frank Mwaisumbe wakati alipokutana na Wasimamizi wa mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali (NGO’S) zaidi ya 30 ili kuyatambua pamoja na shughuli
zinazofanywa na mashirika hayo
Amesema kuwa baadhi ya mashirika yamekuwa chanzo kikubwa
cha migogoro kwa wananchi kwa kujingiza katika siasa na kusahau lengo la kazi
walizojisajili katika kuwatumikia wananchi husika.
Mwaisumbe amesema kuwa serikali inapenda kushirikiana na
mashirika hayo hasa pale yanapofuata utaratibu na sheria zilizoelekezwa na
serikali bila kuvunja utaratibu uliopo katika miongozo inayowaelekeza.
Ameongeza kuwa hapendi kusikia shirika lolote limefutiwa
usajili kwasababu miongozo inawaelekeza shughuli zao wanazotakiwa kuzitekeleza
bila kuathiri wananchi pale wanapotekeleza majukumu yao.
Kwa upande msaidizi wa meneja mradi wa kuwekeza kwa
wanawake wa Kimasai Esther Elias Laly amemshukuru mkuu wa wilaya kwa kukaa
pamoja na mashirika hayo kwa kuwa lazima kuwepo kwa mahusiano baona yao na
serikali.
Ameongeza kuwa kinachotakiwa kwa mashirika hayo kutimiza
masharti yaliyowekwa na serikali ikiwemo kulipa kodi pamoja na kujiepusha na
siasa kwa kuwa nyingine zinajitokeza kipindi cha siasa pekee.
Kwa upande wa Esuphati Ngorupa amesema kuwa kila shirika
lifuate utaratibu waliojiwekea ili lisipelekee kufutiwa usajili kwa kuwa
wameaminiwa na serikali ili washirikiane kuletea wananchi maendeleo.
Dc Longido "Tutazifuta NGO's Zote ambazo hazifanyi kazi yeyote na Zinazojingiza Kwenye Siasa"
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment