Mkazi wa Stendimpya, Mugumu, Nyamhura Werema
(35)amepandishwa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kwa kosa la kumbaka
mtoto wake wa miaka(12)
Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo,
Ismael Ngaile, mwendesha mashtaka wa polisi, Paskael Nkenyenge amesema kuwa
mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai mwaka huu.
“Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba
158(1) (a) cha kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,”
amesema
Amesema Upelelezi haujakamilika na mshitakiwa amekana
shitaka
Mshtakiwa amenyimwa dhamana na kesi yake itatajwa tena
Septemba mwaka huu
Apandishwa kizimbani kwa kumbaka mtoto wake wa miaka 12
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment