Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imejenga vituo
vya afya 108 na inatarajia kujenga vingine 68 katika mwaka huu wa fedha
Ametoa kauli hiyo leo Julai 17, wakati akizungumza na
wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo cha afya cha
Chela, kata ya Chela katika Halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama, mkoani
Shinyanga
Ameipongeza kamati ya ujenzi ya kijiji pamoja na watumishi
wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia vizuri ujenzi na kupata majengo yenye viwango
kupitia "Force Account." Baadhi ya Halmashauri hutumia njia ya
manunuzi ya “Force Account” badala ya kutumia wakandarasi ili kupunguza gharama
na kukamilisha mradi ndani ya muda mfupi
"Majengo haya yamegharimu Sh400 milioni, hongera
wananchi na kamati ya ujenzi iliyosimamia hapa. Tumepata majengo mazuri kwa
sababu ile kamati na watumishi wa Halmashauri ni waaminifu, ndiyo maana majengo
yanapendeza," amesema
Waziri Mkuu alise kuna ombi la zahanati lilitolewa na mmoja
wa wabunge wa viti maalum wa mkoa huo lakini akatumia fursa hiyo kuwapa
mwongozo wananchi kwamba ujenzi wa maboma ya zahanati hivi sasa unafanywa na
wananchi na Halmashauri inamalizia kwa kutoa vifaa vya kuezekea
"Tuna vijiji zaidi ya 16,000 kwa nchi nzima na
tumesisitiza kila kijiji kiwe na zahanati. Tumeamua wananchi wajitolee kujenga
boma na Halmashauri itamalizia kwa kutoa vifaa vya kiwandani kama mabati
na misumari."amesema
Amesema wanahitaji kujenga nyumba ya vyumba vinne ili
wapate chumba cha mganga, chumba cha kufunga vidonda, cha sindano na cha
kutolea dawa
"Serikali yenyewe inaenda kwenye kata na kujenga vituo
vya afya vyenye uwezo wa kutoa huduma zote ili wananchi wasipate taabu ya
kusafiri hadi makao makuu ya wilaya," amesema
"Kila kituo cha afya kinapaswa kiwe na maabara, chumba
cha daktari, cha upasuaji, chumba cha kujifungulia akinamama wajawazito na
chumba cha kupumzikia mama na mtoto. Pia kuwe na chumba cha sindano, vidonda na
kutolea dawa," alisema
Awali, mbunge wa Jimbo la Msalala, Ezekiel Maige
amesema wananchi wa kata hiyo wanakabiliwa na ukosefu wa soko la dengu, hali iliyosababisha
bei ishuke sana.
"Wananchi wa
kata ya Chela ni wazalishaji wakubwa wa dengu na msimu ukiwa mzuri, bei ya
gunia moja inafikia sh. 200,000. Lakini sasa hivi, imeshuka hadi chini ya sh.
100,000. Tunaomba watafutiwe soko ili uchumi wa hapa uinuke," alisema
Akiwa Chela, Waziri Mkuu alimtambulisha Mkuu mpya wa Wilaya
ya KahamaAnamringi Macha ambaye ameanza kazi leo hii baada ya kuapishwa na Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack
"Nimtambulishe kwenu Mkuu mpya wa Wilaya ya Kahama
ambaye hajafikisha hata saa mbili tangu alipoapishwa asubuhi hii. Tayari
ameanza kazi, na hii ndiyo Serikali ya Hapa Kazi Tu," amesema
Waziri Mkuu asema serikali imejenga vituo vya afya 108
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment