Tarime. Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Tarime, Newton Mongi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa
ya chama hicho wilayani humo, Richard Tiboche wanashikiliwa na polisi kwa amri
ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla
Amri ya kukamatwa kwa viongozi na makada hao wa CCM
ilitolewa na Waziri huyo jana Julai 16,2018 wakati wa ziara yake ya kukagua
maeneo yenye migogoro kati Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa) na vijiji vya
kata za Nyanungu, Gorong’a na Kwiwamcha wilayani Tarime
“RPC (Kamanda wa Polisi mkoa) mtie mbaroni huyo kiongozi wa
UVCCM kwa kuitukana Serikali. Mkuu wa mkoa mnakaaje na watu kama hawa;
mwajiriwa anayelipwa mshahara wa CCM anawezaje kuitukana Serikali ya chama
ambacho yeye ni mtumishi wake?” aliamuru Dk Kigwangala na kuongeza
“Nimemsikia kwa maskio yangu akiitukana Serikali ya CCM
ambayo yeye ni kada na kiongozi wake. Kamata na afikishwe mahakamani.”
Amri hiyo ilitekelezwa mara moja na askari polisi
waliokuwepo kwenye msafara huo kwa kiongozi huyo kuwekwa chini ya ulinzi huku
mwenzake ambaye hakuwepo eneo hilo wakati huo alikamatwa baadaye
Hata hivyo, hakujulikana mara moja maneno yaliyotamkwa na
viongozi hao wa CCM yaliyotafsiriwa na Waziri Kigwangala kama matusi kwa
Serikali.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Athuman Mkilindi
ambaye yuko kwenye ziara ya Waziri amesema hajui makosa yaliyosababisha amri ya
kuwatia mbaroni makada hao wa chama kutolewa na kushauri atafutwe Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe kwa ufafanuzi kwa sababu
ndiko makosa yalikotendeka
Mwananchi lilipomtafuta Mwaibambe alisema makada hao
wanashikiliwa na uchunguzi dhidi yao unaendelea
“Ndiyo yuko kwenye uchunguzi lakini inadaiwa kuwa
alimkashifu Waziri wa Maliasili,” alisema
Kigwangala aamuru makada wa CCM Tarime kutiwa mbaron
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment