Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ameonyesha kushangazwa na mila na tamaduni ya kucharazana bakora kwenye jamii
ya washirazi katika kijiji cha Mwaka Kogwa, Makunduchi Kusini visiwani Unguja,
Zanzibar.
Mapigano hayo yaliyodumu kwa masaa
matatu yalishuhudiwa wananchi ambao walipigana kwa fimbo za majani ya migomba
kama ishara ya mila na tamaduni za kijiji chao.
Akizungumza baada ya kushuhudia
sherehe hiyo, Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa amepigwa na mshangao
mkubwa kuona namna ambavyo wananchi hao wanavyopigana huku wakiwa na furaha.
"Ni kweli sijapata kuona namna
ambavyo watu wanachapana viboko namna hii huku wakiwa na furaha, hii ni mara
yangu ya kwanza kuona ",
amesema Majaliwa.
Amesema utamaduni kama huo unajenga
msingi mzuri wa maisha na kusisitiza kuwa kuduumisha kwake ni kuvirithisha
vizazi vijavyo.
Waziri mkuu Majaliwa pia amesema
utamaduni ni fursa nzuri ya kiuchumi hasa ikizingatiwa kuwa sherehe hizo
zinahudhuriwa na watalii kutoka sehemu mbalimbali Duniani.
Sherehe hizo hufanyika kila mwaka
katikati ya mwezi Julai na Agosti, ikiwa inahusisha kuimba nyimbo na kucheza
ngoma zinazoashiria kutakiana mafanikio mema miongoni mwa watu wa jamii hiyo
katika mwaka husika.
Waziri mkuu apigwa butwaa kuona mila hii
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment