Mirerani. Baada ya Tume ya Madini iliyoundwa na Rais John
Magufuli kubaini utoroshwaji wa madini ya Tanzanite katika mji mdogo wa
Mirerani, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Manyara imezuia magari kuingia
ndani ya ukuta huo unaozunguka migodi ya madini hayo
Jana gazeti hili la Mwananchi lilimnukuu mwenyekiti wa tume
hiyo, Profesa Idris Kikula akisema kuwa utoroshaji wa madini hayo ya vito
umesababisha mrabaha kushuka kutoka Sh444 milioni hadi Sh40 milioni kwa mwezi
Hadi kufikia saa 7:00 mchana jana, magari yaliyokuwa
yamebeba maji pamoja na yaliyobeba wachimbaji na wanunuzi yali zuiwa kuingia
migodini
Pia, wachimbaji wadogo walizuiwa kutumia lango hilo kuingia
migodini, wakitakiwa kuonyesha vitambulisha vya Taifa na vile vinavyotolewa na
Wizara ya Madini, hali iliyoibua mtafaruku kutokana na wengi kutokuwa navyo
Tume ya Madini yashtushwa makusanyo Mirerani kushuka
Kwa siku nzima ya Jumatano, kamati ya ulinzi na usalama
ikiongozwa na mkuu wa mkoa huo, Alexander Mnyeti, kamanda wa polisi, Agostino
Senga na mkuu wa wilaya ya Simanjiro Zephania Chaula, ilikuwa eneo la mgodi
kufanya kikao
Mmoja kati ya wamiliki wa migodi ya Tanzanite, Abubakary
Mwamba alisema wachimbaji wadogo wamekwamishwa kufanya kazi yao kutokana na
masharti hayo ya kutakiwa kutotumia magari kuingia na kuonyesha vitambulisho
hivyo
"Magari yameshindwa kupita kwenye lango kutokana na
utaratibu huo mpya wa upekuaji. Tumeambiwa kuwa wizara imeagiza hali hii,"
alisema Mwamba.</p></div><div><p>Alisema Serikali
inapaswa kujipanga kwanza ili kufanikisha zoezi hilo kuliko kuanza kutaka
vitambulisho vitumike ilihali bado hawajajiandaa vya kutosha
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini wa Manyara
(Marema), Sadiki Mneney alisema hawapingi hatua ya Serikali kufuatilia mapato
kupitia migodi hiyo, ila utaratibu unapaswa kuwekwa vizuri
"Wachimbaji wengi hawana hivyo vitambulisho vya Taifa
na vilivyotolewa na wizara na vitambulisho vya mpigakura havitakiwi
kutumiwa," alisema Mneney
Alisema wachimbaji hawapingi zoezi hilo kwa kuwa lina
manufaa kwa Taifa katika kufuatilia mapato, lakini akaitaka iweke utaratibu
vizuri.
Hata hivyo, bado
vifaa vya ukaguzi, upekuzi na taa zilizoahidiwa kuwekwa na Rais Magufuli wakati
wa uzinduzi wa ukuta huo, bado hazijawekwa
Hivi sasa, askari polis,i maofisa madini na maofisa wa Idara
ya Usalama wa Taifa ndiyo wanalinda lango kuu kwa kuhakikisha wanawatambua
wanaoingia na wanaotoka migodini.
Kuingia Mirerani sasa kwa vitambulisho vya Taifa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment