Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira),
Anthony Mavunde ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora kuanza
mchakato wa kukirudisha serikalini kituo cha vijana cha Tulu ambacho
kinamilikiwa na asasi ya Pathfinder
Amesema haiwezekani asasi isiyo ya kiserikali itumie fedha
za Serikali, akitaka mchakato huo uanze mara moja ili kirudi Serikalini, lakini
akataka vijana wapatao 36 waliopo kituoni hapo wawekwe kwenye mpango wa
kunufaika na kituo hicho kitakaporudishwa serikalini badala ya kufukuzwa
Akizungumza leo Julai 18, 2018 katika kituo hicho kilichopo
Kata ya Igigwa, Mavunde alisema anashangazwa kuona kituo kinapewa na Serikali
Sh1.8 bilioni halafu matumizi yake hayaeleweki
Mavunde alisema kiasi kinachodaiwa kutumiwa ni kikubwa na
kutaka uchunguzi wa kina ufanyike kujua matumizi ya fedha hizo
"Jengo kama là ukumbi na ofisi kumi kugharimu Sh200
milioni si sahihi. Ingawa mimi si mhandisi, lakini kwa macho unaona,"
amesema
Mavunde ameonyesha masikitiko yake kwa kituo hicho kutumika
vibaya huku viongozi wakihusika kuvuruga malengo ya kituo hicho ya kuwapa
vijana mafunzo ya ujuzi kama ushonaji, ufundi useremala na uashi.
Mavunde aicharukia Halmashauri ya Sikonge
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment