Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangala ameagiza
wafugaji wanaoishi eneo la malisho katika kijiji cha Nyichoka wilayani hapa
kuhama mara moja
Akiwa eneo ambalo simba tisa waliuawa kwa sumu Mei 31 katika
eneo la malisho ya kijiji cha Nyichoka, Dk Kigwangalla amesema wafugaji
wanaoishi maeneo hayo ndiyo waliohusika na hujuma hiyo
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini
hapo leo Julai 17, DK Kigwangala amesema wavamizi hao wanatakiwa kuondoka
kuanzia sasa kwa kuwa kijiji hicho kimepimwa na kina mpango wa matumizi bora ya
ardhi
“Hapa ninyi ni wanufaika wakubwa wa uhifadhi kwa kuwa ninyi
mnaunda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ikona, eneo la malisho
mmekaribisha wafugaji hatuwezi kukubali kubadili matumizi ya mpango ambao
umewawezesha kuunda jumuiya hii," amesema.
Ameagiza taasisi zote za uhifadhi kutumia sheria ya
kutaifisha mifugo inayokamatwa ndani ya hifadhi, badala ya kupiga faini ili
kukomesha wanaochungia ndani ya maeneo hayo
"Ukilea nyani utavuna mabua na sisi sasa tunatakiwa
tubadilike kwani tumekuwa wapole, wameteketeza familia nzima ya simba ambao
wana mchango mkubwa wa uchumi,"amesema na kuongeza
“Sitakubali simu za wabunge, mwenyekiti au katibu wa CCM kwa
hili. Kama mnatafuta kura hizi hazifai maana chama chetu hakikubaliani na
hujuma kama hizo.”
Amesema maliasili inachangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la
taifa na mifugo inachangia asilimia nne
“Kwa mtu mwenye akili lazima awekeze kwenye pato kubwa.
nasema tena sasa ni mwendo wa kutaifisha ili tuweze kulinda maliasili
tuliyopewa na Mungu kuitunza,”amesema
Awali, mkurugenzi wa uhifadhi wa Shirika la Hifadhi la Taifa
(Tanapa), Martin Loibooki amesema chanzo cha migogoro katika maeneo ya hifadhi
ni kushindwa kusimamia kanuni za uendeshaji ikiwamo usimamizi wa matumizi bora
ya ardhi
Naye mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu ameagiza
kufikia Agosti 15 wafugaji wote wanaoishi maeneo ya malisho wawe wameondoka
"Waziri hili niachie mwenye akili aanze kuondoka
kuanzia sasa, kwa kuwa itakapofika muda huo itakuwa uvungu kwa uvungu nyumba
kwa nyumba aliyekuuzia eneo mtajuana wenyewe," amesema
Waziri Kigwangala atua kijiji walichokufa Simba tisa, aamuru wafugaji eneo hilo wahame
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment