Benki ya NMB imehukumiwa kulipa jumla ya Sh12 milioni baada
ya kuipa kazi kampuni ya Kalongo’s General Supply ambayo haijasajiliwa na Bodi
ya Usajili wa Makandarasi (CRB
Wakati benki hiyo ikihukumiwa kutoa kiasi hicho kutokana na
makosa matatu iliyothibitika kuyatenda, mkurugenzi wa kampuni hiyo ya
ukandarasi, Japhet Sanga ametakiwa kulipa Sh3 milioni kutokana na kujipatia
kazi kinyume na utaratibu uliowekwa kisheria
Akisoma hukumu hiyo leo, Julai 17, hakimu mkazi mfawidhi wa
mahakama hiyo, Michael Mteite amesema NMB imekutwa na makosa matatu likiwamo la
kumpa kazi mkandarasi ambaye hajasajiliwa na CRB
Makosa mengine ni kukaidi tahadhari iliyotolewa na CRB na
kutotii agizo lililoitaka benki hiyo kutoendelea na kampuni hiyo na
kuweka mifumo ya kuzuia na kuzima moto kwenye matawi ya benki hiyo yaliyopo
Nyanda za Juu Kusini.
“NMB ina hatia kwa
makosa yote matatu na itatakiwa kulipa faini ya Sh4 milioni kwa kila kosa ndani
ya siku 30 na ikishindwa kufanya hivyo mahakama itaamuru meneja wake kwenda
jela miaka mitatu kwa kila kosa na adhabu hiyo itatumikiwa kwa wakati mmoja,”
alisema Hakimu huyo
Kifungo cha miaka mitatu jela pia kitamuhusu Sanga endapo
atashindwa kulipa faini aliyopewa na mahakama hiyo
NMB yahukumiwa Sh12 milioni kwa kukiuka taratibu za kikandarasi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment