Wagombea 11wa udiwani wa Chadema, wameenguliwa katika
uchaguzi mdogo kwa sababu kadhaa ikiwamo kutokujua kusoma na kuandika
Miongoni mwa wagombea walioenguliwa wapo watano wa wilaya ya
Ngorongoro
Madiwani 19 wa Chadema walijiuzulu nafasi zao na kujiunga na
CCM, huku diwani mmoja wa chama hicho kata ya Baray, Moshi Darabe, akifariki
dunia. Darabe alikuwa pia Mwenyekiti wa chama hicho Karatu
Akizungumza leo Julai 17, Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa
Arusha, Aman Golugwa amesema kuenguliwa kwa wagombea wake 11 kumetokana na
mizengwe ya uchaguzi na vitisho kwa wagombea
"Hadi sasa ni kweli tumebaki na wagombea 9 tu kati ya
kata 20, maeneo yote tulitaraji kuwa na wagombea lakini, wamejiondoa dakika za
mwisho, wengine kung'olewa eti hawajui kusoma na kuandika na wengine vitisho
hawajarejesha fomu,"amesema
Amesema katika jiji la Arusha ambapo kunatarajiwa uchaguzi
wa kata nne, pia kuna wagombea wawili wa kata ya Osunyai na Kaloleni wamewekeza
mapingamizi na tayari yamejibiwa
"Huu uchaguzi utakuwa mgumu sana tayari tumelalamika
tume ya taifa ya uchaguzi na polisi, kuna sehemu mgombea wetu aliambiwa
kuandika jina la zinjanthropus na alipokosea akaondolewa eti hajui kusoma na
kuandika, mwingine amenyang'anywa fomu mlangoni "amesema
Hata hivyo, Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha, Shaban
Mdoe amesema chama hicho, kimejiandaa kurejesha kata zote na wagombea wa
Chadema wengi wamejitoa baada ya kubaini hawatoshi katika nafasi walizoomba na
hivyo kuwaachia wa CCM
"Kuna mapingamizi yamewekwa kihalali na wengine
wamejitoa baada ya kubaini hawajui kusoma na kuandika," amesema
Hata hivyo, wasimamizi wa uchaguzi mkoani Arusha, wote
walieleza taratibu zote kufuatwa katika uchaguzi, ikiwamo kuenguliwa wagombea
wanaokosa sifa
Msimamizi uchaguzi wilaya ya Longido ambapo uchaguzi
ulipangwa kufanyika katika kata tatu, Jumaa Mhina amesema katika halmashauri
yake mgombea mmoja wa Chadema kata ya Alang'atadapash Isaya Laizer hakurejesha
fomu
Mhina amesema katika kata ya Kamwanga mgombea wa
Chadema Sakimba Alais pia aliwekewa pingamizi kwa tuhuma za kutojua kusoma
Msimamizi jimbo la Ngorongoro, Raphael Siumbu amesema katika
kata tano, wagombea wanne wa CCM wamepita bila kupingwa
Amezitaja kata hizo kuwa ni Soitsambu, Pinyinyi, Ngoile na
Ngorongoro ambapo kata moja ya Alaitole ndio kulikuwa na mgombea ambaye pia
baadaye alijitoa
Katika halmashauri ya Monduli, Msimamizi wa uchaguzi, Stevin
Ulaya amesema kati ya kata sita, mbili wagombea wa CCM wamepita
bila kupingwa
Ulaya amesema wagombea wa Chadema waliochukua fomu
hawakurejesha katika kata za Nararami na Loksale na kata nyingine taratibu za
uchaguzi zinaendelea
Katika uchaguzi huo CCM iliwapitisha kugombea madiwani
wote 19 wa Chadema waliojiuzulu na kujiunga na CCM
Wagombea udiwani Chadema waenguliwa kwa kutojua kusoma, kuandika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment