Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha imendelea kuboreka kwenye
masuala ya Elimu baada ya miradi ya Elimu yenye Garama ya zaidi ya shilingi
bilioni 3 kuletwa kwa kipindi cha miaka miwili na Nusu na katika Fedha Hizo sh
Bilioni 1 zitajenga Shule ya sekondari ya wasichana katika kata ya Laitole
Wilayani Humo.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye
pia ni Naibu waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Mh William Olenasha wakati
akizungumza na wananchi wa kata ya Esere katika muendelezo wa Ziara yake ya
kutembelea wananchi ili kuwaeleza mafanikio aliyoyapata tangu alipopata nafasi
ya kuongoza wananchi wa Jimbo la Ngorongoro.
Olenasha ambaye tangu amechaguliwa na wananchi wa jimbo
lake kwa miaka miwili na nusu amefanikiwa kuboresha Elimu na mpaka sasa kwa
kipindi hicho shule za Msingi 6 zimejengwa na Sekondari Tatu ambapo ni juhudi
hizo ni kati yake na wananchi waliomchagua pamoja na ushirikiano wa Serikali ya Raisi Dokta John Magufuli .
Olenasha ambaye tangu ameanza ziara hiyo ametembelea jumla
ya kata 13 za jimbo lake amesema kuwa tayari eneo la kujenga shule
limeshapatikana na wataalamu wa halmashauri wanaoshughulika na masuala ya Ardhi
wameshaagizwa kwenda kupima eneo hilo na ujenzi utaanza hivi karibuni.
Amesema kuwa Elimu ya mtoto wa kike itakuwa bora zaidi
kwasababu kilio cha mtoto wa kike kuendelea na masomo kitakua kimesikika.
“Kilio cha watoto wa kike ambao hawaendelei kwenye shule
ngazi za juu kimesikika sasa Ngorongoro siku hizi ndiyo vijana wanasoma lakini
watoto wa kike wamebaki nyuma tumeona kwamba tuwaanzishie shule maalum ambayo
ni ya wasichana na na mmebahatika shule hiyo kiwilaya hiyo itakuwa kata ya
Laitole Kijiji cha Esere”Amesema Olenasha
Olenasha amesisitiza kuwa mradi huo ni wa pekee kuja
katika kata hiyo ya Laitole hivyo ni vizuri wananchi wakasimamia vizuri kwa
kushirikiana pindi mradi huo utakapoanza kwa ajili ya manufaa ya watoto ili
kupata wasomi wa baadae kwasababu mabadiliko makubwa yanakuja.
Mosses Lekui mwananchi wa Wilaya ya Ngorongoro amesema
kuwa uwepo wa shule hiyo ya sekondari ya wasichana itakayoanza kujengwa hivi
karibuni itasaidia jamii ya kifugaji kupeleka watoto wa kike shule na kupata
elimu bora ya maisha yao ya baadae.
Amesema wanafunzi wanatembea umbali mrefu kufuata shule
za sekondari baada ya kumaliza darasa la saba lakini ujio wa mradi huo
utawapunguzia hata wao garama za kuwapeleka watoto wa kike shule za mikoa ya
mbali ambapo pia ni garama kubwa.
Awali Mbunge wa Ngorongoro Mh William Olenasha akiwa
ameongozana na katibu wa Bunge walifika Eneo litakalojengwa Shule hiyo ya
Sekondari ya wasichana ambayo itasaidi kwa kiasi kikubwa watoto wa kike
kuendelea na masomo yao.
Shule ya Sekondari ya Wasichana Kujengwa Wilayani Ngorongoro
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment