Mwandishi wetu,Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla
amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini, kujiandaa kuondoka
ndani ya miezi mitatu kabla ya operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu kuanza.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika eneo la hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori(WMA) ya
Makao, wilayani Meatu, Dk Kigwangalla alisema wavamizi wa maeneo ya hifadhi
wengi wamekuwa wakijihusisha na matukio ya ujangili.
"Utakuta kijiji kina ardhi kubwa, lakini wengine
wanajenga hadi katika ndani ya eneo la mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na hao
mara nyingi ndio wanaingiza mifugo hifadhini usiku na kufanya ujangili,"
alisema
Alisema maeneo mengi ya hifadhi na mapori ya akiba
nchini yamevamiwa na wananchi jambo ambalo serikali haiwezi kukubali yaharibiwe
ama kutumika kwa ujangili.
Waziri huyo, pia alitembelea kambi ya kitalii ya Mbono
inayomilikiwa na Kampuni ya Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) na hoteli ya
kitalii ya Mwiba (Mwiba Lodge) na kushuhudia vikosi vya kupambana na ujangili
katika maeneo hayo ambavyo vipo yapo chini ya taasisi Friedkin Conservation Fund (FCF) na kueleza
kuridhishwa na uwekezaji wa taasisi hiyo.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Mwiba Holding, Abdulkadir
Mohammed, alisema katika eneo la Mwiba wamewekeza sh 2.2 bilion na hivi sasa
wanaendelea na shughuli za uhifadhi na utalii.
"Mheshimiwa Waziri katika eneo hili, kampuni yetu
inafanya utalii wa picha na kuna hoteli, tunafanyakazi kwa amani na utulivu na
vijijini vinavyotuzunguka," alisema.
Mwenyekiti wa kijiji cha Makao, Anthony Philip, alimweleza
Waziri Dk Kigwangalla kuwa, katika eneo hilo kuna mahusiano mazuri baina ya
vijiji na wawekezaji na vijiji vinapata mgao wa fedha.
Philipo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwangudo alisema
kijiji cha Makao kimekuwa kikipata zaidi ya Sh 147 milioni kwa mwaka kutoka kwa
mwekezaji na vijiji vingine sita vimekuwa vikipata zaidi ya milioni 80,000 kila
mwaka.
Akiwa katika pori la akiba la Maswa, Meneja wa pori
hilo, Lusato Masinde alisema pia wanauhusiano mzuri na wawekezaji ambao licha
ya kulipia ada za vitalu pia wamekuwa wakitoa msaada wa huduma mbali mbali
ikiwepo maji.
Hata hivyo, alisema katika pori hilo changamoto kubwa ni
uvamizi wa mifugo, uchache wa watumishi
na upungufu wa vitendea kazi.
Waziri Dk Kigwangalla ataka wavamizi maeneo yaliyohifadhiwa kuondoka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment