Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Songwe
kwa ziara ya siku tano itakayojumuisha kufungua kituo cha afya Nanyala na
kuweka jiwe la msingi, mradi wa maji wa Iyula
Taarifa iliyotumwa leo Julai 21 kwa vyombo vya habari na
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, imeeleza kuwa Makamu wa Rais amepokelewa na
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala pamoja
na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na MichezoJuliana Shonza na Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga na Viongozi wengine wa Chama na
Serikali
“Akiwa mkoani Songwe, Makamu wa Rais atakagua na kuhamasisha
shughuli mbalimbali za maendeleo ambapo atatembelea Wilaya Tatu za Mkoa huo
ambazo ni Mbozi, Momba na Ileje,” imesema taarifa hiyo
Makamu wa Rais ataanzia ziara yake katika Wilaya ya Mbozi
ambapo miongoni mwa shughuli atakazofanya ni pamoja na kukagua na kufungua
kituo cha Afya Nanyala, kusalimia wananchi katika eneo la mradi la Nanyala,
kuweka jiwe la Msingi katika Mradi wa maji Iyula na kufanya Mkutano wa hadhara
katika kijiji cha Iyula
Makamu wa Rais pia atatembelea Wilaya ya Momba ambapo
atakagua na kuzindua kituo cha Afya Tunduma, atakagua shughuli za vikundi vya
wajasiriamali Tunduma na kufanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wananchi wa
Wilaya ya Momba
Vilevile, Makamu wa Rais atatembelea Wilaya ya Ileje ambapo
atapokea taarifa ya shughuli za uhifadhi wa mazingira na upandaji miti na
kukagua shughuli za uhifadhi na shamba la miti la Wakala wa Misitu
Tanzania lilopo Katengele na baadae kufanya mkutano wa hadhara katika
kijiji cha Isoko ambapo atapata fursa ya kuzungumza na wananchi wa Ileje.
Makamu wa Rais kufanya ziara ya siku tano Songwe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment