Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa
Kilimanjaro, Anna Mghwira amemtaka Kamanda wa Polisi mkoani humo kumchukulia
hatua za kinidhamu Mkuu wa Kituo cha Polisi Mwanga na askari wa kituo kidogo
cha polisi Nyumba ya Mungu na Lang'ata wilayani kutokana na tuhuma za
rushwa dhidi yao
Mghwira ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,ametoa
agizo hilo leo Julai 21,wakati akizungumza kwenye mkutano wa Hadhara katika
Kata ya Lang'ata,Wilaya ya Mwanga
Katika Mkutano huo ambao, uliohudhuriwa na Katibu wa Itikadi
na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, na viongozi wengine wa chama na
serikali,Mghwira amesema Askari hao wamekiuka taratibu na kujiingiza kwenye
vitendo vya rushwa,hatua ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika jitihada za
kudhibiti uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu
Amesema Askari hao wamejianzishia vituo vyao vya ushuru na
kuanza kukusanya mapato yatokanayo na uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya
Mungu,ambalo lilifungwa baada ya kukithiri kwa uvuvi haramu na samaki kupotea
"Naomba niseme Askari wa Lang'ata na Nyumba ya Mungu
mmenikwaza,kwani kituo chenu kipo juu na mtu hata awe mfupi kunizidi anaweza
kuona mazingira yote ya Bwawa na kuona wavuvi haramu,lakini wao huwa
hawawaoni, hii ni hatari sana,naomba RPC uwaondoe mara moja na
kuwachukulia hatua,"amesema Mghwira
Mkuu huyo ambaye alitangaza kulifungua Bwawa la Nyumba ya
Mungu kwa Muda,alisema serikali ilikuwa na nia njema kulifunga Bwawa hilo,lakini
Askari wamepoteza malengo ya serikali na kukwamisha mpango wa kuacha
samaki wawe wakubwa
Akizungumza katika kikao hicho, Polepole alisema serikali
haitawavumilia askari au watendaji watakaobainika kujihusisha na vitendo vya
rushwa na kuchafua utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya Tano
Mghwira amuagiza kamanda wa polisi kuwachukulia hatua Mkuu wa kituo, polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment