Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dk Faustine Ndugulile
amegoma kuzindua chuo cha Udaktari Musoma baada ya kuhisi kuna matumizi mabaya
ya fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho kilichopo
mjini Musoma
Badala yake,
ametoa wiki mbili kwa Mkuu wa Chuo hicho, Dominic Tarasa kuandika maelezo
na mchanganuo wa matumizi ya zaidi ya Sh500 milioni zilizotumika kwenye mradi
huo
Akizungumza
baada ya kutembelea chuo hicho mjini Musoma leo Julai 21, Dk Ndugulile amesema
ubora wa majengo ya chuo hicho hauakisi thamani ya fedha zilizotimika kuzijenga
na kuzikarabati miaka miwili iliyopita
"Majengo
yamejaa nyufa huku rangi ikionekana kupauka miaka miwili pekee ya ujenzi;
Hakuna value for money (thamani ya fedha). Siwezi kushiriki uhalifu huu na
lazima wahusika watoe maelezo ya kutosha," amesema Dk Ndugulile
Naibu Waziri
huyo amesema matumizi ya aina hiyo yanakwamisha ufanisi katika utekelezaji wa
mpango wa Serikali ya kuboresha huduma katika sekta ya afya
Akizungumzia
matumizi ya fedha na ubora wa majengo, Tarasa amesema kazi ya ujenzi na
ukarabati ilisimamiwa na kuthibitishwa na wataalam kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto
"Ushiriki
wangu katika mradi huu ulikuwa ni kupokea majengo," amesema Tarasa
Waziri Ndugulile agoma kuzindua chuo cha udaktari Musoma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment