Na
Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha
Askari
Polisi wa kike mkoani hapa ambao pia ni wanachama wa TPF NET wamepongezwa
kutokana na utendaji wao wa kazi katika nyanja mbalimbali ndani ya Jeshi la
Polisi.
Hayo
yameelezwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi alipokuwa anafungua mafunzo ya siku mbili
kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika Chuo cha Mafunzo cha Cyprus Hill
kilichopo Monduli.
Kamanda
Ng’anzi alisema kwamba askari hao wameweza kushika nyazifa mbalimbali ikiwemo
kuwa wakuu wa upelelezi na wakuu wa vituo ngazi ya wilaya mfano Monduli
na Arumeru na hata katika ofisi mbalimbali ambapo wamefanya kazi kwa uaminifu
na uadilifu.
Alisema
kwamba mifano hiyo itawafanya askari wa vyeo vya chini waweze kujiamini zaidi
na semina hiyo itakuwa chachu ya kuwaongezea maarifa katika utendaji wao wa
kazi za kila siku pamoja na kuwawezesha kutoa maamuzi sahihi wakati wote.
Kamanda
Ng’anzi alisema kwamba askari hao wa kike si bora tu kwenye utendaji wa kazi za
ndani ya nchi lakini pia baadhi yao wamewahi kuiwakilisha vyema nchi yetu
kulinda amani katika nchi mbalimbali ikiwemo Sudani
Aliwataka
askari hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuzidi kusonga mbele
zaidi kimadaraka huku akitolea mfano wa baadhi ya Makamanda wa Polisi wanawake
katika baadhi ya mikoa lakini pia Kamishna Mstaafu wa Jeshi hilo (CP) Alice
Mapunda.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mtandao huo mkoani hapa, Mrakibu wa Polisi (SP)
Namsemba Mwakatobe alisema kwamba lengo la mafunzo hayo ambayo yalihudhuriwa na
washiriki 45 toka wilaya zote za mkoa huu ni kukumbashana wajibu wao katika
utendaji wa kazi za kila siku lakini pia kubadilishana uzoefu ili kila mmojawao
atimize wajibu wake ipasavyo.
Alisema
Mtandao huo pia umeweza kuanzisha mfuko wa kusaidiana pindi mmojawao anapopata
matatizo ambapo askari wengi wa kike wanajitokeza hali ambayo inaonekana
kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao.
Aidha
kwa upande wa Madawati ya Kijinsia na Watoto Mwenyekiti huyo alisema kwamba
wameweza kufanya vizuri hasa katika utoaji wa elimu juu ya unyanyasaji lakini
pia kuwadumia wananchi kwa kiwango bora katika ofisi zao.
Naye
Mtaalamu wa Jamii ambaye anahusika na mafunzo katika kituo cha Cyprus Hill cha
shirika la Masai Stoves Bi. Meesha Kingolyo alisema kwamba, wao waliamua
kujitolea kusaidia mafunzo hayo ili baadae jamii ipate elimu na kuondokana na
mfumo dume ambao kwa kiasi kikubwa umewaaathiri wanawake na watoto ambapo
baadhi yao hawapati masomo.
Alisema
anaamini mara baada ya mafunzo haya jamii itakuwa na muamko juu ya usawa wa
jinsia ambapo pia itasaidia wanawake na watoto wapate haki zao za kimsingi
lakini pia anategemea kwamba kesi zitakazofikishwa Polisi zitasimamiwa vyema.
TPF NET ARUSHA YAPONGEZWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment