Waendesha Bodaboda jijini Arusha wamelalamikia kutekwa na
kuuawa wanapokuwa kwenye mazingira ya kazi zao huku wakiiomba Serikali
kukomesha mauaji hayo pamoja na kuchukuliwa hatua kwa wale wanaobainika
kuhusika na mauaji hayo.
Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Kata ya
Muriet iliyopo mkoani Arusha, AKILI MBAGA mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mh.KANGI LUGOLA wakati wa ziara ya kikazi katika kituo cha Polisi
Muriet ambapo Waziri LUGOLA alipata pia fursa ya kusikiliza kero za wananchi
hao
Akijibu swali la Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Kata ya
Muriet, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.KANGI LUGOLA, katika kudhibiti
matukio ya utekwaji na mauaji hayo, ametoa maagizo kwa Inspekta Jenerali wa
Jeshi la Polisi kumuandalia takwimu za mauaji hayo ya madereva bodaboda kwa
miaka mitano nchi nzima ili Serikali iweze kubaini maeneo sugu ya mauaji hayo
na iweze kujipanga kudhibiti mauaji hayo
Waendesha Bodaboda wawashtaki watekaji kwa Waziri Lugola
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment