Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 31, 2018 itawasomea
maelezo ya awali viongozi tisa wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho,
Freeman Mbowe
Hayo yameelezwa leo Jumatano Julai 25, 2018 na hakimu mkazi
mkuu wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri ambaye pia ameutaka upande wa
utetezi ukiongozwa na wakili Nashon Nkungu kwamba ukiwa na hoja ya kutaka kesi
hiyo iahirishwe kwa muda mrefu, uziwasilishe
Uamuzi huo umetolewa baada ya wakili wa Serikali Mkuu,
Faraja Nchimbi kuieleza mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa
Nchimbi ameifahamisha mahakama hiyo kuwa Julai 20, 2018
Mahakama Kuu ilitoa uamuzi wake katika maombi ya marejeo namba 126 /2018
yaliyowasilishwa na washtakiwa kwa kuyatupilia mbali kwa sababu yalikosa vigezo
vya kisheria na pia iliona maombi hayo yalikuwa ni batili
Kutokana na mazingira hayo, ameiomba mahakama kuipangia kesi
hiyo tarehe nyingine ya usikilizwaji wa maelezo ya awali, baada ya hapo ipange
tarehe ya kuanza kusikilizwa mfululizo kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa
mashtaka.
Wakili Nkungu kwa niaba ya wakili Peter Kibatala na Jeremiah
Mtobesya ameitaarifu mahakama hiyo kuwa Julai 20, 2018 Mahakama Kuu
iliyatupilia mbali maombi ya marejeo namba 126/2018 na kwamba baada ya uamuzi
huo walionyesha nia ya kukata rufaa na wameshapeleka kusudio la kukata
rufaa Mahakama Kuu siku hiyo hiyo
Baada ya Nkungu kueleza hayo, Wakili Nchimbi amedai amesikia
hoja lakini kwa kuwa hazijawekwa katika kumbukumbu za mahakama ameomba kesi
ipangiwe tarehe nyingine
Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza hoja za upande zote
ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 31, 2018
Hata hivyo, wakati kesi hiyo inaendelea washtakiwa Mbowe na
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji hawakuwepo mahakamani baada ya
kupata hudhuru
Washtakiwa waliokuwepo mahakamani leo ni naibu makatibu
wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar), mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche; mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Bunda Mjini,
Ester Bulaya
Wengine ni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na
mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13,
ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za
chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa
la jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018 jijini Dar es Salaam
Vigogo Chadema kusomewa maelezo ya awali Julai 31
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment