Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), limesema kauli ya
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ya
kukihusisha Chadema na mauaji ya mwanafunzi Akwilina Akwiline, inalenga
kukiwekea chama hicho vikwazo kwenye uchaguzi mdogo wa Agosti 12
Akizungumza na wanahabari jana, Kamanda Mambosasa alisema
askari waliokuwa wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na kifo cha mwanafunzi wa
chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) waliachiwa huru baada ya ushahidi kuwa
hafifu
Mambosasa alinukuliwa akisema, badala yake waliohusika ni
Chadema waliohamasishaji maandamano yale ya kisiasa yaliyofanyika Februari 16,
siku moja kabla ya uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni.<
Akwilina alipigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala
wakati viongozi na wanachama wa Chadema wakiandamana kwenda Ofisi ya Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Kinondoni
Akizungumza na wanahabari leo Julai 25, Mwenyekiti wa
Bavicha Patrick Ole Sosopi amesema kauli ya Mambosasa inalenga kuwaaminisha
wananchi kuwa shughuli za Chadema ni hatari na sio salama kwa watu kuhudhuria
"DPP (Mkurugenzi wa mashtaka) alishafunga jalada la
kesi ya Akwilina, lakini Mambosasa ameliibua upya tena wakati ambao tunaelekea
katika uchaguzi ili kuonyesha kuwa maandamano yanasababisha mauaji. Propaganda
kama hizi alitakiwa kuzifanya Polepole (Katibu Mwenezi wa CCM) na sio mtendaji
wa chombo cha dola," amesema Ole Sosopi
Amesema hata leo yakiitishwa maandamano ya nchi nzima kama
polisi hawatumii nguvu kuyazuia, hayawezi kusababisha mauaji kwa kuwa mtu hafi
kwa kuandamana bali kwa kusababishiwa kifo hivyo polisi wafanye uchunguzi wa
kutosha
"Anasema viongozi wa Chadema waliokuwepo pale walikuwa
na silaha, kama wao ndiyo walihusika waseme ni silaha ya nani iliyotumika kwani
kuna maganda yaliyookotwa? Hivyo uchunguzi ukifanyika mhusika atabainika lakini
katika mkutano ule polisi ndiyo waliokuwa na silaha za kivita," amesema
Ole Sosopi
Pia wametoa wito kwa wanafunzi wote nchi nzima na wazazi
kulilia damu ya Akwilina mpaka pale haki itakapotendeka, lakini pia wao
wataandika barua kwa balozi zote hapa nchini kuzitaarifu kuhusu hali ya
ukandamizaji wa haki za binadamu ili wachukue tahadhari wawapo hapa.</
Chadema wamshukia Kamanda Mambosasa kifo cha Akwilina
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment