Serikali imepokea gawio la Sh717.56 bilioni kutoka kwa
kampuni, taasisi na mashirika ya umma kwa ajili ya mwaka 2018
Akizungumza katika hafla ya kupokea gawio hilo leo Julai 23,
2018 jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka amesema gawio
hilo ni kutoka kwa kampuni, taasisi na mashirika ya umma 43 kati ya 90 ambayo
yanastahili kutoa gawio
Mbutuka amesema changamoto iliyopo ni kuwa kuna baadhi ya
kampuni zisizozingatia ubia baina yao na Serikali. Amesema zipo ambazo
hutangaza kutoa gawio kwa wanahisa lakini hushindwa kuwasilisha serikalini
Msajili amesema viwanda vingi vimekuwa vikisuasua akieleza
kati ya 51 vilivyofungwa 12 vilikiuka masharti ya mkataba na wawekezaji wake
hawakuonyesha nia ya kuviendeleza
Amesema Hazina imetoa ilani kwa wawekezaji tisa kuonyesha
nia ya Serikali kuvitwaa viwanda na kuviendeleza
“Ubinafsishaji ulikuwa na nia ya kuongeza tija na
isitafsiriwe kama tunafanya utaifishaji, tutavichukua, tutatangaza na kuwapa
wawekezaji wengine ili kutimiza shabaha tuliyojiwekea,” amesema
Amesema viwanda vitatu vimerejeshwa serikalini na wawekezaji
wengine wamepewa
Serikali ya Tanzania yapokea gawio la Sh717.6 bilioni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment