Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametoa saa
24 kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Sokoni, Kata ya Tandale, Murshida
Diswela kuripoti kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni
Diswela ambaye ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anadaiwa
kukusanya fedha za wananchi zaidi ya Sh1 milioni kwa ajili ya kuzibua mifereji,
lakini hadi leo hakuna utekelezaji uliofanyika
Pia, Hapi amemwagiza ofisa ustawi wa jamii wa kata ya hiyo,
Naomi Kasekenya kufanya uhakiki ili kubaini vijana walioandikishwa na kulipwa
fedha za miradi ya kusaidia kaya maskini kupitia Tasaf, huku wakiachwa wazee na
wenye uhitaji huo
Hapi ameyasema hayo leo Julai 23, 2018 katika siku ya kwanza
ya ziara yake ya kutembelea kata zote 20 za wilaya hiyo ya jijini Dar es Salaam
Wananchi wakitoa kero zao kwa Hapi, wamesema Diswela
aliwachangisha Sh40,000 kwa kila kaya kwa ajili ya kuzibua mifereji iliyopo
eneo hilo, lakini wanapofuatilia hawapewi jibu na mwenyekiti huyo
"Nakuagiza kamanda wa polisi huyu mwenyekiti kufikia
kesho awe amejisalimisha na atoe maelezo yanayojitosheleza fedha za wananchi
amezipeleka wapi, hivyo akija na maneno matupu mwekeni ndani," amesema
Hapi
Mkazi wa eneo hilo, Asha Mkunya amesema tangu mwaka 2015
walichangishwa fedha hizo ambapo kwa eneo hilo la Bondeni walitoa Sh400,000 na
wanaokaa karibu na sokoni zaidi ya Sh500,000
Pia amesema fedha za Tasaf baadhi ya viongozi wamekuwa
wakigawana wenyewe huku wakiwaandikisha ndugu zao ambao hawastahili kupewa na
kuwaacha wazee wenye uhitaji
Amesema atawaagiza watu kutoka ofisini kwake ili waende
kuhakiki kwenye kata hiyo, hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria
Ofisa mtendaji wa kata hiyo, Athuman Mtono amesema suala
hilo aliligundua wiki iliyopita wakati wakifanya usafi alipelekewa malalamiko
kuwa wenyeviti wa serikaki za mitaa wamekuwa wakiingiza watu wao na kuwaacha
wazee ambao wanatakiwa kupata fedha za Tasaf
DC Hapi ampa saa 24 mwenyekiti wa mtaa kujisalimisha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment