Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndungulile ameuagiza
uongozi wa hosptali ya mkoa wa Simiyu kumrudishia mara moja pesa zake mama
mmoja mkazi wa bariadi ambaye amelazwa katika wodi ya watoto baada ya kumueleza
waziri kuwa aliambiwa na manesi kuwa akanunue maji kwa ajili ya kumtundikia
mwanae ambaye anaumwa.
Dkt.Ndungulile ametoa Kauli hiyo wakati alipotembelea
hospitali hiyo na kuonana na wagonjwa mbalimbali ambapo akiwa katika wodi ya
watoto alimuuliza mama huyo kuhusu huduma alizopata na mwanae ambaye pasipo
kuficha alimuambia kuwa aliambiwa akanunue maji ya Drip kwa pesa yake katika
maduka ya nje.
Aidha Naibu Waziri huyo ameuagiza uongozi wa mkoa Simiyu
kuwatafuta watu wanaoishi na VVU waliocha kutumia dawa za kufubaza makali ya
virusi zaidi ya elfu kumi pamoja na ongezeko la vifo vya wakinamama wajawazito
ambapo pia ametaka kufahamu mikakati ya mkoa katika kuangalia tatizo la idadi
kubwa watu wanaokatisha dawa za kurefusha maisha ili waweze kukabiliana nalo
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameahidi kushirikiana
na wadau mbalimbali kuwahimiza wananchi kupima kwa hiari VVU ili mkoa uweze
kutokomeza kabisa ugonjwa huo.
Dkt Ndungulile Ataka Mama alienunua Dripu kwa pesa yake Kurudiswa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment