Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace
Karia amesema kuwa ongezeko la wachezaji kumi wa kigeni ni makubaliano baina ya
timu husika za ligi na bodi ya ligi
Karia ameyasema hayo leo alipozungumza na waandishi wa
habari kuhusu ongezeko hilo na kusema kuwa klabu zenyewe ndiyo zilizopendekeza
kuongeza wachezaji kutoka saba hadi kumi
Karia amefanya hivyo baada ya wadau akiwemo Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe kutoa maoni ya
kupinga uamuzi huo uliochukuliwa na TFF
Karia amesema klabu za ligi kuu kupitia kwa aliyekuwa
mwenyekiti wao wa bodi ya ligi (Clement Sanga) walikutana katika kikao cha
Tarehe 30 juni 2018 katika ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa kuzungumzia
masuala kadhaa likiwemo suala la kanuni mpya za ligi kuu
"Viongozi wa klabu pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa
Bodi ua Ligi walikutana katika kikao kilichokuwa kinazungumzia masuala
mbalimbali yakiwemo ya kanuni mpya za ligi kuu na katika hayo pia waliweza kujadili
ongezeko la wachezaji kutoka saba mpaka kumi na wakafikia makubaliano ya
pamoja,"amesema Karia
Karia ameongeza klabu zenyewe ndiyo zilipendekeza ongezeko
la wachezaji wa kigeni kutoka saba mpaka wachezaji 10. Mapendekezo ya Kanuni
yalijadiliwa katika Kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF na wakakubaliana na
hoja za ongezeko hilo katika Ligi kuu na kupitisha maombi yao
RAIS WA TFF AFAFANUA ONGEZEKO LA WACHEZAJI WA KIGENI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment