UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili
Mhasibu Mkuu wa bodi ya Pamba Tanzania Simon Maganga umeieleza Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, upelelezi dhidi ya kesi hiyo bado haujakamilika
Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), Maxi Ali ameeleza hayo leo Julai 24 mwaka 2018 mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Janeth Mtega, kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa
Wakili Maxi amedai mahakamani hapo kuwa, kesi ilipangwa kwa
ajili ya kutajwa.Upelelezi wake bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe
nyingine ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la
Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo
hadi Agosti 23 mwaka 2018
Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka manne ya
matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajili,moja la ufujaji na
ubadhilifu na uhujumu uchumi kwa kusababisha hasara ya Sh 55,637,680
Katika shtaka la kwanza mshtakiwa huyo wanadaiwa
kuwa kati ya Januari Mosi, 2009 na Desemba 31,2010 katika ofisi ya bodi ya
Pamba Tanzania iliyopo Wilaya ya Ilala akiwa mtumishi wa umma,
Mhasibu Mkuu kwa lengo la kumdanganya mwajiri wake
Ambapo alitumia vocha za kuwasilisha mbegu za pamba msimu wa
2009/2010 akijaribu kuonesha kampuni ya Afrisian Ginning Ltd ilinunua mbegu za
Pamba kilo 25,129,258k wakati wakijua si kweli
Katika shtaka la pili anadaiwa kuwa katika kipindi
hicho,mshtakiwa huyo akiwa na lengo la kumdanganya mwajiri wake alitumia vocha
za kuwasilisha mbegu za Pamba msimu wa mwaka 2009/2010 akijaribu kuonesha
kampuni ya Nyanza Cooperative Ltd ilinunua kilo 3,708,998 za mbegu za Pamba
wakati akijua si kweli
Katika shtaka la tatu,Maganga anadaiwa katika kipindi hicho,
akiwa na lengo la kumdanganya mawajili wake alitumia vocha za kuwasilisha mbegu
za pamba msimu wa mwaka 2009/2010 akijaribu kuonesha kampuni ya kampuni ya
S&C Ginning Ltd ilinunua kilo 17,152,590 za mbegu za pamba
wakati akijua si kweli
Katika shtaka la nne, mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa
katika kipindi hicho akiwa na lengo la kumdanganya mwajili wake alitumia vocha
za kuwasilisha mbegu za Pamba msimu wa mwaka 2009/2010 akijaribu kuonesha
kampuni ya kampuni ya Kahama Oil Mill Ltd ilinunua 16,326,038 za
mbegu za Pamba wakati akijua si kweli
Wakati katika shtaka la tano, mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa
katika kipindi hicho akiwa katika ofisi ya bodi ya Pamba Tanzania, alifanya
ufujaji na ubadhilifu wa Sh 55,637,680 mali ya aliyopewa na bodi ya Pamba
Tanzania
Pia mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi mwaka
2009 na Desemba 31 mwaka 2010 akiwa Mhasibu Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania kwa
makusudi aliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 55,637,680
USHAHIDI DHIDI YA KESI MHASIBU MKUU BODI YA PAMBA BADO HAUJAKAMILIKA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment