CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) kimezindua rasmi tuzo ya
Mwajiri Bora kwa mwaka 2018 ili kutathmini
mchango wa rasimali watu kwa kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika utendaji
wa masuala mbalimbali ya kibiashara
Tuzo ya Mwajiri Bora (EYA) lilianzishwa mwaka 2005 na
kuendeshwa kila mwaka na chama cha waajiri Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt Aggrey Mlinuka amesema kwamba
tuzo ya mwajiri bora wa mwaka imelenga zaidi kuwatambua wanachama waliofanya
vizuri katika kuweka mikakati bora yenye kutathmini usimamizi wa rasilimali
watu na shughuli za kibiashara
Dkt Mlinuka amesema kwa miaka kadhaa tuzo hizo zimehamasisha
makampuni wanachama kuweka juhudi katika masuala ya ajira na usimamizi wa
rasilimali watu kama msingi mkakati wa makampuni yao kujenga nguvu kazi yenye
ujuzi, furaha, ushindani na yenye kushiriki kikamilifu katika uzalishaji
Amesema, kutokana na maoni yaliyotolewa na wanachama, wadau
na wataalamu mbalimbali tuzo ya mwajiri bora kwa mwaka jana ilihusisha tuzo 8
zaidi ili kuendana na mazingira ya kibiashara kwa sasa ikiwemo uwiano wa kazi
na maisha, mwajiri bora ni yule anayesimamia vema nguvu kazi inayoonekana
kupotea, waajiri bora ni wenye mikakati inayojali afya za waajiri
Mengine ni tuzo ya utofautishwaji na ushirikishwaji, waajiri
bora ni wanaowachochea na kuwajali waajiriwa wenye ujuzi, waajiri bora wenye
mahusiani mazuri baina ya waajiri na waajiriwa, waajiri bora wenye majina
makubwa na imara huvutia wateja, waajiri, wadau na mwajiri bora ni yule
aliyewekeza kwenye teknolojia
Ameeleza kuwa, tuzo hizo zinasimamiwa na kampuni ya
TanzConsult inayoongozwa na Prof Beautus Kundi na wanachama watatakiwa kuanza
kujaza fomu hizo kupitia tovuti ya tuzo ya waajiri ambapo baadae mwaka huu
Mwezi Desemba mshindi atapatikana
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri (ATE) Dkt Aggrey Mlinuka
akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa tuzo ya Mwajiri bora kwa
mwaka 2018 itakayofanyika Desemba
MCHAKATO WA TUZO ZA MWAJIRI BORA WAANZA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment