Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa
habari alipokutana nao hii leo Jijini Dodoma
Waziri Mhagama ametengua Bodi ya Shirika la Mfuko wa Taifa
wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Utenguzi huo umeanza hii leo tarehe 24 Julai, 2018,
baada ya hatua mbalimbali za Serikali ya Awamu ya Tano kuendelea kuimarisha
utendaji kazi wa Taasisi na Mashirika yake
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB)
alipokutana na waandishi wa habari hii leo Mjini Dodoma Julai 24, 2018
Waziri Mhagama alieleza kuwa, kwa mujibu wa mamlaka
aliyonayo kama Waziri wenye dhamana kwenye masuala ya hifadhi ya jamii
ninatangaza rasmi kuivunja Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii pamoja na uteuzi wa Wajumbe wote wa bodi hiyo
Lengo kuu la madiliko haya ni kuhakikisha kuwa shirika hilo
linaimarishwa zaidi sambamba na kusimamia mwenendo wa kila siku wa shirika
ikiwemo zile kazi za msingi kuongeza wanachama, kukusanya michango, kulipa
mafao kwa wakati na kusimamia vitega uchumi kwa uzalendo na weledi alisisitiza
Mhe. Mhagama
Aidha, Waziri Mhagama alitoa taarifa rasmi kuhusu mfumo
utakao tumika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya Mashujaa ambayo hufanyika
tarehe 25 Julai kila mwaka. Katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli, fedha zilizopangwa kufanyia maandalizi ya sherehe hizo
Kitaifa ambazo ilikuwa zifanyike kwenye Jiji la Dodoma zitatumika kuboresha
miundombinu ya barabara katika Jiji la Dodoma
Mwaka huu 2018 hakutakuwa na maadhimisho ya pamoja ya siku
ya kumbukumbu ya mashujaa, baadala yake kila Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji
watafanya maadhimisho ya siku hiyo kwa kufanya usafi katika maeneo waliyozikwa
Mashujaa wetu na maeneo yoyote ambayo yanakumbukumbu za Mashujaa wetu nchini alisema
Mhe. Mhagama
WAZIRI MHAGAMA ATENGUA BODI YA NSSF
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment