Serikali imemsimamisha kazi Mhandisi wa maji wa wilaya ya
Korogwe mji Joseph Mcharo kwa tuhuma za kushindwa kusimamia vyema fedha za
miradi ya maji wa gharama nafuu na na kusababisha maelfu ya wakazi kuhangaikia
huduma hiyo usiku na mchana kuwaacha
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
kijiji cha Msambiazi kilichopo kata ya Mtonga wilayani Korogwe naibu waziri wa
maji na umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso amesema serikali ya Mheshimiwa John Pombe
Magufuli imeanza mchakato wa kuwafukuza kazi baadhi ya wahandisi nchini ambao
wamekuwa mzigo badala ya kusaidia wananchi
Katika mkutano huo ulihudhuriwa na watendaji wwa
halmashauri,na wananchi wachache wa eneo hilo ,mkuu wa wilaya ya Handeni
anayekaimu nafasi hiyo kwa wilaya ya Korogwe amemuhakikishia naibu wwaziri kuwa
fedha za mradi wa maji wa Msambaiazi kiasi cha zaidi shilingi milioni 134
atazisimamia ipasavyo badala ya kuwaacha wataalam
Kufuatia hatua hiyo naibu waziri Aweso amemuagiza mkurugenzi
halmashauri ya wilaya Korogwe mji kuwaeleza wananchi kuhusu fedha hizo huku
akimtaka mkandarasi kueleza ni lini mradi huo utakamilika
Mhandisi wa maji Korogwe asimamishwa kazi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment