Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro
Mambosasa amesema askari waliokamatwa wakihusishwa na kifo cha aliyekuwa
mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini
wameachiwa huru
Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa
risasi kichwani akiwa kwenye daladala eneo la Mkwajuni jijini hapa, wakati
polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema
Aprili 20, 2018 Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo
Mganga alisema jalada la kesi ya Akwilina amelifunga rasmi, kubainisha kuwa
Jeshi la Polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano au vurugu na kusababisha
mauaji, haliwezi kushtakiwa
Leo Jumanne Julai 24, 2018 wakati akizungumza na waandishi
wa habari baada ya kuulizwa hatima ya askari hao, Mambosasa amesema wameachiwa,
“ni kweli kuna askari tulikuwa tunawashikilia kwa ajili ya uchunguzi, upelelezi
ulipomalizika imebainika hawahusiki.”
“Wale askari waliachiwa kwa maelekezo ya mwanasheria na ushahidi
ulikuwa hafifu wa kuwatia hatiana.”
Awali, Mambosasa amewaonya watumiaji wa barabara kuwa makini
na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa madereva wazembe hususan wa
bodaboda ambao hawatii alama za barabarani
Pia amezungumzia watuhumiwa wawili wanaoshikiliwa kwa tuhuma
za kuhujumu mawasiliano ya Shirika la Mwasiliano Tanzania (TTCL).
Amewataja watu hao kuwa ni Kelvin Same, mkazi wa Tabata
Segerea ambaye ni mfanyakazi wa TTCL kitengo cha huduma kwa wateja na Lilian
Hosea ambaye ni mkazi wa Mbezi Beach na mhasibu wa shirika hilo
Amebainisha kuwa Julai 12, 2018 walipata taarifa kutoka kwa
ofisa upelelezi wa TTCL kuwa kuna wafanyakazi wa shirika hilo
wanajihusisha na udukuzi wa data za kampuni kutoka taasisi za Serikali
zinazotumia mtandao wa TTCL.
Taasisi hizo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Maendele ya Jamii (Tasaf),
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA
Amesema watumishi hao wamesabishia hasara ya Sh46 milioni na
kwamba uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani
Polisi waliohusishwa mauaji ya Akwilina waachiwa huru
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment