JESHI la Polisi mkoa wa Arusha linawashikilia watu 40 kwa tuhuma
mbalimbali za matukio ya uhalifu mkoani Hapa.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha,Ramadhani,Ng’azi, amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo mbalimbali na taratibu
zinakamilika
ili kuwafikisha mahakamani.
Amesema katika tukio la kwanza jeshi la Polisi limewakamata watu
wawili wakiwa na kilo 98 za Mirungi wilayani Longido ambazo zilikuwa ziikingizwa nchini .
wawili wakiwa na kilo 98 za Mirungi wilayani Longido ambazo zilikuwa ziikingizwa nchini .
Katika tukio lingine watuhumiwa wanane wamekamatwa na misokoto 18 ya bangi kwenye kijiji cha Mto wa Mbu wilayani Monduli.
Kamanda Ng’azi,amesema katika tukio lingine jeshi la polisi limekamata Malori 20 pamoja na madereva wake 20 na wamiliki wa malori hayo wapatao 20 na
watafikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kutumia vyombo vya usafiri vyenye
ubovu.
Polisi Arusha yawashikilia watu 40 kwa matukio yabuhalifu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment