Jeshi la Polisi Arusha. Lataka dereva asiye na cheti cha udereva aache gari akasome


Jeshi la Polisi Mkoani Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Veta limezindua mafunzo ya muda mfupi kwa madereva wa magari ya abiria na utalii na kuonya madereva wasio na vyeti vya udereva watachukuliwa hatua Kali ikiwemo kufutiwa leseni zao.

Akifungua Mafunzo hayo kwa madereva 260  kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ,Ramadhani Ng'anzi amesema Mafunzo hayo yanalenga kuwapatia Elimu ya darasani kwa madereva wa mabasi ya abiria kwa lengo la kupunguza ajali zinazotokana na madereva wasiozingatia sheria za usalama barabarani.

Amesema jeshi hilo limejipanga kuanza msako mkali kwa madereva ili kuhakikisha madereva wote  wamepitia mafunzo ya darasani na kupata vyeti halali vya udereva. 

Naye Abraham Mbuguni,ambaye ni Mratibu wa Mafunzo ya muda mfupi kutoka veta Arusha,amesema kuwa Mafunzo hayo mafupi yanatolewa kwa muda wa  wiki mbili,katika awamu hiyo ya 132.

Amesema kuwa wanafunzi hao watafanyiwa majaribio Agosti3 mwaka huu ambapo aliomba Jeshi hilo kuweka utaratibu wa namna ya washiriki hao kuweza kuendelea na kazi ya udereva katika kipindi hiki cha Mafunzo cha muda wa wiki mbili ili waweze kuhudumia familia zao.

Amesema katika Mafunzo hayo mada mbalimbali ikiwemo Elimu ya usalama barabarani,ukaguzi wa Gari na ufundi,sheria za usalama wa barabarani,nyaraka za usafirishaji na uchukuzi na udereva wa kujihami.

Kwa upande wake Mkuu wa Usalama Barabarani ,RTO Joseph Bukombe,amesema madereva wanapaswa kutambua kuwa serikali inapodhamiria kufanya jambo,haitasita na kuwa operesheni ya kukagua madereva wenye vyeti itakuwa endelevu.

Kuhusu manyanyaso kwa madereva,RTO aliwashauri madereva hao wa magari ya abiria kuwa na chama chao ili wamiliki wa magari wawe wanachukua madereva kutoka kwenye chama chao na Jeshi la Polisi litawapa ushirikiano katika suala hilo.

"Iwapo mtakuwa na chama chenu kitawasaidia kuwabana wamiliki wa magari wenye tabia ya kuwapa magari mabovu na kutishia kuwafukuza madereva chama hicho kitawasaidia madereva," amesema
Jeshi la Polisi Arusha. Lataka dereva asiye na cheti cha udereva aache gari akasome Jeshi la Polisi Arusha.  Lataka dereva asiye na cheti cha udereva aache gari akasome Reviewed by KUSAGANEWS on July 26, 2018 Rating: 5

No comments: