Jeshi LA Polisi Mkoa wa Arusha Kwa kushirikiana na Bodi ya Michezo ya
Kuhatisha Tanzania(GBT)imekamata na kuteketeza Mashine Feki 45 zenye
thamani ya sh,milioni 90 za Michezo ya
kubahatisha ziizoingizwa nchini kinyemela na kutokuwa na usajiri.
Akiongea na Vyombo vya habari
lleo Julai 26 Kamanda
Wa Polisi Mkoa Wa Arusha,Ramadhani Ng'anzi amesema Mashine hizo zilikatwa
maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha katika operesheni ya wiki moja
iliuofanyika.
Aidha amesema katika operesheni hiyo watu wawili wanashikiliwa na
poliao akiwemo raia wa China wakihusishwa na uingizaji na uuzaji wa Mashine
hizo bila kufuata utaratibu ikiwemo kutosajiliwa na bodi, kutokulipa kodi
ya serikali huku zikitumika maeneo ambayo hayajaidhinishwa.
Kwa upande wake,meneja wa ukaguzi na udhibiti wa bodi ya Michezo ya
kubahatisha nchini,Sadick Mangesho amesema kuwa awali bodi hiyo ilipata taarifa
za kuingizwa kinyemela kwa Mashine hizo bila kufuata utaratibu wa usajiri huku
baadhi yake zikiwa ni feki.
Amesema Mashine hizo zimesambazwa katika maeneyo mbalimbali
yasiyoidhinishwa na zinatumika kuibia wananchi na zimekuwa zikiendeshwa bila
kulipia kodi ya serikali.
Amesema baadhi ya wamiliki wa Mashine hizo walifanikiwa kutoroka ila
walifanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wawili akiwemo RAIA wa China na mtanzania
Mmoja .
Hata hivyo upelelezi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.
Zoezi la operesheni linaendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini
ambapo hivi karibuni walikamata na kuteketeza Mashine zaidi ya 80 mkoani
Kigoma.
Amesema kuwa Mashine hizo zinapoingia nchini huwa wanaziweka alama maalum za utambuzi ambazo zinaonyesha zinastahili kutumika nchini na zimesajiliwa na bodi hiyo.
Naye Afisa utamaduni wa halmashauri ya Jiji la Arusha,Benson
Maneno,alipongeza maafisa hao kwa kushirikiana nao kuendesha operesheni hiyo na
kuwa wao kama Jiji walishaanza operesheni na kuhakikisha hakuna Mashine feki
inayotumika.
Mashine feki za Bahati nasibu yateketezwa Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment