Mwapulise Mwafikwa (28) anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji
ambaye alitoroka akiwa chini ya ulinzi katika mahakama ya Wilaya ya Njombe
mkoani Njombe amekamatwa na polisi mkoani Dodoma
Mwafikwa anakabiliwa na kesi ya mauaji namba PI 08/2015
ambapo pia anadaiwa aliwahi kufungwa jela kwa kosa la kupatikana na silaha
Akizungumza kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto
amewaeleza waandishi wa habari kuwa mshatakiwa huyo alikamatwa Julai 24, 2018
Amesema baada ya kutoroka alijificha katika mashamba Kiteto
Mkoani Manyara na katika kiijiji cha Ngomai Wilaya ya Kongwa
Kamanda Muroto amesema kuwa mshtakiwa huyo atasafirishwa
kwenda Wilayani Njombe ili kuendelea na kesi yake ya mauaji pamoja na
kufunguliwa shtaka la kutoroka akiwa chini ya ulinzi
“Kwa kuwa taarifa za kutoroka kwake zilienea maeneo mengi
mkoani hapa watu wema wasiopenda uhalifu walifanikisha kumkamata mtuhumiwa na
kumfikisha kituo cha polisi Kibaigwa,”amesema
“Nawapongeza wananchi waliofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa
huyu hatari, niwaombe waendelee kutoa ushirikiano kwa polisi.”
Mshtakiwa wa mauaji aliyewatoroka polisi Njombe, adakwa Dodoma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment