IMEBAINIKA
kuwa watoto wa kike 36 kati ya 100 huolewa chini ya umri wa miaka 18 nchini
Tanzania huku ikichangiwa na sababu mbalimbali ikiwepo hali duni ya umaskini
pamoja na tamaa hali inayopelekea kuongezeka kwa matukio ya ukatili dhidi ya
watoto.
Hayo yamebainishwa
na Mwenyekiti wa mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni (TECMN) Valerie Msoka alipokua katika mkutano
uliowashirikisha wajumbe wa baraza la mahusiano ya dini mbalimbali.
Amesema kuwa,
Licha ya juhudi mbalimbali ambazo wamekua wakizichukua ili kutokomeza tatizo
hilo lakini bado kuna haja ya
kurekebishwa sheria ya ndoa ya 1971 kifungu cha (13) (17) kinchoruhu ndoa chini ya umri wa miaka 18
ambapo imekua ni tatizo kubwa katika kuongezeka kwa vitendo vya ukatili.
Kwa upande
wake Mratib wa mtandao huo, Michael Jackson
amesema kuwa,wamekua wakifanya utafiti kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa maendeleo pamoja na kuonesha matamasha mbalimbali ambayo yamekua
yakilenga kutoa elimu juu ya athar zinazopatikana kwa ndoa za utotoni.
Aidha amesema kwa
majibu wa utafiti uliofanywa na mtandao huo umeonesha kuwa, Tabora kati ya
watoto 100 watoto 58 wameolewa chini ya umri wa miaka 18, Shinyanga 59,Mara 55
pamoja na Dodoma 51 hali ambayo hupelekea kuathirika kwa watoto kisaikolojia na
kimwili.
Naye Sheikh
Hassan Chizenga Katibu wa baraza la ulamaa Bakwata amesema kuwa yeye kwa majibu
wa Dini ya Kiislam haoni kama kuna haja ya kubadishwa sheria hiyo kwani mtoto
anaruhusika kuolewa baada ya kubaleghe, kama shida ni umri zifungishwe kwa
kufuata sheria na utaratib maalum.
Hali Duni ya Maisha yasababisha watoto Chini ya Umri wa miaka 18 Kuolewa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment